Mtaalam wa maswala ya ngono nchini Kenya Maurice Matheka amepinga dhana kwamba misimu ya baridi huchochea kuzaliwa kwa watoto wengi.

Katika mahojiano na BBCswahili, mtaalam huyo anasema kwamba fikra hiyo imetumiwa na wanaume kama chambo cha kuwavutia wanawake katika mazungumzo wakati wa msimu wa baridi.

Matheka anasema kuwa Waafrika wamelelewa katika tamaduni ambazo zinawafanya kuhisi kana kwamba mkutano wowote wa mume na mke katika eneo la faragha huchochea kufanyika kwa mapenzi.

”Ni kweli kwamba misimu ya baridi huwachochea wanaume na wanawake kukumbatiana ,lakini swala kwamba hatua hiyo inaweza kuchochea ngono sio la kweli. Wenzetu wazungu kwa mfano wana misimu ya baridi lakini hilo halitokei”, alisema mtaalamu huyo.

”Msimu wa baridi humuathiri mwanamume na hivyobasi yeye hutaka joto mwilini lakini sio kwamba watu wanapokumbatiana husababisha kufanyika kwa tendo la ngono”.

Mtaalam wa maswala ya kingono nchini Kenya Maurice MathekaMtaalam wa maswala ya kingono nchini Kenya Maurice Matheka

Hatahivyo utafiti unasema kwamba unapotaka kukabiliana na homa wakati wa msimu wa baridi basi shiriki tendo la ngono.

Kulingana na utafiti uliochapishwa na BBC, wataalam wa maswala ya kisaikolojia wamedhihirisha kwamba watu wanaotekeleza tendo la ngono mara moja ama mbili kwa wiki kinga zao hupata nguvu zaidi.

Dr Carl Charnetski, wa chuo kikuu cha Wilkes University mjini Wilkes-Barre, na mwenzake Frank Brennan walichunguza kuhusu athari za ngono katika kinga ya mwanadamu .

Waliwahoji wanafunzi 111 kutoka chuo kikuu cha Wilkes walio kati ya umri wa miaka 16 hadi 23, kuhusu ni mara ngapi wameshiriki ngono mwezi uliopita.

Pia walipima kiwango cha kinga yao katika mate.

Kulingana na mwanasayansi huyo, matokeo yalibaini kwamba wanafunzi waliotekeleza ngono chini ya mara moja kwa wiki walikuwa na kiwango cha juu cha kinga ikilinganishwa na wale ambao hawakushiriki kabisa.

Chanzo: BBC