Je unamfahamu mwanariadha mwenye mafanikio makubwa Zanzibar?

 Michezo ni miongoni mwa nyenzo kuu na muhimu ambayo huifanya jamii kuwa bora kiakili ,kimwili na hata kuleta maendeleo kwa taifa pamoja na mahusiano ya karibu baina ya mtu na mtu au taifa kwa taifa.

   Sio tu kama michezo huleta mambo hayo bali na hata kumfanya mtu kujijengea manufaa na kipato  sambamba na kupata ajira na kujipatia mahitaji yake ya kila siku ,kama tunavyo waona vijana katika nchi mbalimbali  ulimwenguni wanavyo jinyakulia mafanikio kupitia michezo .

   Na kwaupande wa Zanzibar vijana wengi  kwa sasa wanajishughulisha na michezo kama ni kazi au kibarua chengine, wengi wao wameshafanikiwa na michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu ,mbio za riadha  ,mpira wa kikapu na michezo mengineyo.

  Miongoni mwa kijana aliepata mafanikio kupitia michezo ni kijana mmoja mchapa kazi ,mwenye kufanya kazi bila kusukumwa na pia huifanya kwa hima na wala hana huruma  anachotaka kusimamia .

  Ni wingi wa bidii,mbinu,maarifa pamoja na kufanya kila liwezekanalo ilimradi kupata analohitaji katika mchezo wake ambao ndio tegemeo kwake na hufanya kazi kwa moyo mkunjufu wala hajali mapungufu tena bila kujenga hofu kwa sasa ni mzoefu.

  Sio hivyo tu pia ni mwenye kasi ya ajabu wala hajenda kwa babu au mbinu za matabibu bali amejengwa akajengeka hii nikutokana na anafanya kazi kwa kupenda  na sio kulazimishwa  ”Amesema mwalimu wake.

  Hufanya kila namna zoezi haachi nyuma kwani wataalamu  wanasema kufanya zoezi kwa sana hukujenga kuwa imara  ,kujiamini na kijipa matumaini ya kupata unacho kikusudia.

Kijana huyo si  mwengine ni Ali Khamis Gulamu,  mwanariadha mashuhuri wa Zanzibar ambaye  anaendelea kuipatia sifa Zanzibar na anaitangaza sekta ya michezo  kwa kiasi kikubwa na kutambulikana kimataifa  kupitia michezo.

 Mwanariadha huyo mkaazi wa Shauri Moyo ambaye amezaliwa  12/07/1990 huko Kianga na amemaliza masomo yake ya kidato cha pili mwaka 2009, pale ilipofika 2010 alipatiwa  ushauri  na  Baba yake Khamis Ghulam  na kumpeleka mazoezi ya riadha kwa lengo la kumfunza ili asije kujiunga na vikundi viovu  na kumfanya  mwanariadha na ije kuwa kazi ambayo itampatia ajira.

  Baba yake ameliona hilo kwa ambali anasimulia Gulam    Mwanariadha huyo alifanya mazoezi ya kujifua kwa  muda wa miaka miwili ndipo hapo 2012 alianza kushiriki mashindano ya vilabu za hapa hapa Zanzibar  Kutokana na kufunya vizuri mwanariadha huyo katika mashindano ya vilabu aliendelea kushiriki sehemu mbali mbali kama vile Tanzania Bara,Kenya ,Uganda ,Kongo na Arusha .

   Anasimulia Ali Gulam: hapo hakuridhika napo aliengeza bidii hadi kushiriki mashindano ya kimataifa yanayo tambulika kimataifa kama vile “All African Games” na  ‘’Comsemas game.’’ na huko kafanya vizuri kama alivotarajia .

   ‘’kupitia mashindano mbali mbali  ya kimataifa ambayo nimeshiriki   nimejifunza mambo mengi sana kama vile watu kujiandaa mapema ,ushirikiano kwa wanafunzi na walimu wa mafunzo ya michezo (makocha) ni mkubwa sana kitu ambacho kinafanya kuleta ushindi kwa urahisi’’amesema Ali gulam.

Mwanariadha huyo aliendelea kuipa sifa Zanzibar na yeye mwenyewe pamoja na klabu yake ya KMKM ambayo ndio iliyomlea na kumuandaa kijana huyo baada ya kumuona ni mwanariadha makini.

   Ali Gulamu mwanariadha  matata  amesema anajivuania kuwa  mwanariadha ambaye anaaminika na klabu yake ya KMKM kwa kazi nzuri anayoifanya  ya kuiwakilisha kimataifa sekta  ya michezo ya Zanzibar  kupitia mchezo wa Riadha na kupata  mafanikio mengi anayojipatia kupitia riadha kama vile kupatiwa Ajira na klabu yake ya  KMKM kujengewa nyumba kujulikana maeneo mengi pamoja kutembea sehemu  mbali mbali za dunia  kama vile China ,Australia ,Kenya ,Uganda ,Congo  pamoja na maeneo mengine mengi.

  ”Kwa sasa namiliki medali takriban 25 ambazo zipo mikononi mwangu na nategemea kupata zaidi na kufika mbali zaidi ya hapa nilipo ili kujipatia manufaa mengi ambayo nimejipangia  kwa malengo yangu ya baadae  “alisema  Ali Khamisi.

   Hata hivyo mwanariadha huyo ambaye hukimbia mbio takribani  mita 100 hadi 200 ambazo hujulikana kama mbio fupi  na  ameeleza kuwa mbio fupi zinahitaji umakini wa hali ya juu ili kupata ushindi mana hutumia nguvu nyingi na pia kila mchezaji anataka ushindi huo huo  kwahiyo inahitaji  umakini wa juu ili kupata ushindi.

  Pia amesema  klabu  haihitaji mchezo huo tu bali wanashiriki michezo tofauti tofauti  ikiwemo mbio ndefu kama mita  800,   1000 na kuendeleaa ,michezo ya urushaji na urukaji zote wanashiriki lakini yeye anapendelea zaidi  mchezaji wa mbio fupi na mara kwa mara ndio anao shiriki na kijipatia ushindi.  Mwanariadha huyo hakukaa kimya aliendelea kutoa maelezo kwa kusema anahakikisha anakuwa mwanariadha maarufu duniani kama alivo ”Usen Bolt” amesema ni mwanariadha anaemkubali sana na anamini ipo siku atamfikia mwanariadha huyo.

  ”Kwa sasa nimejipanga vizuri kimazoezi na nishapelekwa China na kwa ajili ya mazoezi zaidi na jinsi ya kujiandaa kwa mchezo mengine iliyopo mbele yangu na kwasasa nipo sawa kwa mchezo wowote ule” alisema Ali Gulam.

    Mwanariadha huyo ametoa shukrani  kwa mwalimu wake Kassim Hussein mkaazi wa Fuoni ambae pia ni mwalimu msaidizi wa kikosi cha KMKM , amemshukuru kwa kusema bila yakujitihada ya mwalimu asingefika hapo alipofanikiwa sasa hivi .

   Hata hivyo ametoa shukrani kwa serekali kwa kuwa pamoja nao kwa kuwapa misaada mbali mbali pale wanapopata safari za njeya ya nchi

    “Mafanikio huja kwa jitihada ya mchezaji mwenyewe na hata hivyo klabu haiwezi kufika popote bila msukumo wa serekali  na ni vyema kuwa karibu zaidi ili kuitangaza Zanzibar yetu  “ ameeleza mwalimu wa Ali Khamis .

  Na pia Ali hakukaa kimya  aliendelea kusema ijapokuwa amepata mafanikio makubwa katika klabu yake lakini zipo changamoto zinazomkabili zikiwemo changamoto za kukatishwa tamaa ,kuweka kambi kwa muda mrefu ,sambamba na kukosa mahitaji ya lazima au hata vifaa vya kutosha vya kufanyia mazoezi.

    Hivyo Ali  Gulam anaiyomba serekali kuwasaidia kwa kila hali na mali ili wazidi kufanya vizuri na kuitangaza Zanzibar kupitia michezo  ,vile vile amewaomba serekali wawe kitu kimoja ili waweze kufikia malengo yao wali jipangia.

    Mbali na hayo Ali Gulam amewataka vijana wenzake kujishughulisha na michezo ili kujipatia maslahi zaidi ikiwemo  ajira, afya  pamoja na kujifunza vitu vingi kutoka nchi mbali mbali na watu tofau,na tuache  kukaa mitaani na kufanya vtendo viovu  .

Kwa sasa Ali Khamisi Gulam anaishi shauri moyo na familia yake na mke wake na watoto wake bado atabaki kuwa mwanariadha kinara ndani ya Ardhi ya visiwa vya Zanzibar binafsi naweza kumpa jina ‘’Usein Bolt wa Zanzibar ‘’.

Picha:

Na Ibrahim Makame.