Wanaume walioathirika na unyanyasaji wa kijinsia wakiwa watoto katika jamii ya watu weusi wamekuwa wakirudishwa nyuma na serikali, alisema kiongozi mmoja aliyewahi kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wakati akisikiliza wanaume ambao walipitia unyanyasaji wa aina hiyo wakitaka suala lao liangaliwe kwa ukaribu.

” Nimjaribu kusahau lakini nimeshindwa. Nimejaribu kuendelea na maisha yangu lakini bado kitendo cha unyanyasaji nilichofanyika nikiwa mdogo bado kipo akilini mwangu”, alisema ambalo si jina lake la kweli.

Chris aliongea mara baada ya chapisho la serikali nchini Uingereza kuchapisha ripoti likiwa linaelezea namna ambavyo waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia wanavyosaidiwa na serikali.

Nilipokuwa na mika 11, huyo aliyenibaka alikuwa na kiongozi wa shule mwenye umri wa miaka 19.Alikuwa analia wakati anasimulia mkasa wake.

“Nilivyobakwa nilijiona sina thamani tena,”

“Niliugua kwa muda, Nadhani ilikuwa ni sonona ingawa ukiwa mtoto unakuwa uelewi mambo hayo.

“Hilo jambo lilinichanganya sana na kubadilisha utu wangu mpaka leo, ni kovu ambalo ninalo gumu kulikabili.”

Chris anasema bado anaishi katika maumivu. Ilimchukua miaka mingi kutafuta msaada.

“Sikuongea na mtu yeyote kuhusu jambo ambalo nilifanyiwa. Wala sikutoa taarifa kwa vyombo vya sheria.

“Na kwa sababu sikushitaki jambo hilo.”