Jeshi la polis Mkoa wa Mjini Magharib Unguja  bado  linaendelea na operesheni zake za usalama  barabarani ambapo jumla ya makosa 201 yamekamatwa huku makosa 82 yamepelekwa mahakani na kutozwa faini ya sh 2,750,000/= kama ni adhabu.

Akizungumza na wandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polis Mkoa wa Mjini  Magharib Thoubas Gesauda Sedoyeka amesema kuna ajali mmoja ambayo imeripotiwa huku hakuna ajali iliyosababisha kifo kwa wiki hii.

Kwa upande mwengine Kamanda Sedoyeka amesema jumla ya makosa manne ya ukamataji wa bangi ambapo nyongo 5 zimekamatwa ambazo zinasadikiwa kuwa ni banghi.

Pia amesema jumla makosa matatu ya dawa za kulevya   yamekamtwa ambapo jumla ya kete 58 zinazosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya na watuhumiwa wamepelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Sambamba na hayo amesema kwa  upande wa makosa ya udhalilishaji wa kijinsia jumla ya  makosa 3 yameripotiwa  ambapo makosa 3 ni ubakaji  na moja ni la kulawiti hadi sasa hakuna  mtuhumiwa hata mmoja alilyekamatwa  kuhusiana na kesi hizi huku ikiwa upellezi ukiendela.