Jeshi la Polisi laendeleza doria Kaskazini Unguja

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja linaendelea na doria ili kudhibiti vitendo vya uhalifu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, Pombe za kienyeji na makosa mengine.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi Haji Abdalla Haji kufuatia kuwakamata Eliza Juma Fabiani na Ali Mohd Ibrahimu wenye umri wa miaka 27 huko  Kiwengwa wakiwa na kete tofauti 244 na kete 72 zinazosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.

Kamanda Haji ameitaka jamii kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini na kukamata wahalifu wakiwemo wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Kamanda Haji amesisitiza kuwa doria zinazofanyika mkoani humo zina lengo la kulinda usalama wa raia na mali zao.

Rauhiya Mussa Shaaban