Jeshi la Polisi Nchini Uganda limesema lina taarifa kuwa Mgombea Urais kupitia NUP, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ana mpango wa kujifanya ametekwa baada ya kupiga Kura ifikapo Januari 14/2021.

Msemaji wa Polisi, Fred Enanga, amesema inawezekana Mgombea huyo atajificha katika Balozi mojawapo na kisha kudai ametekwa na Maafisa wa Serikali ili kuchochea vurugu zinazofanana na zile zilizotokea Novemba mwaka jana na kusababisha vifo zaidi ya 30