Mbwa wa kazi maalum za Bandari ya Dar es Salaam anayedaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, alikuwa kwenye mafunzo bwalo la Polisi.
Hayo yameelezwa leo Agosti Mosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa katika mkutano na wanahabari. Amezungumza hayo huku ukumbini hapo kukiwa na mbwa wawili wa polisi akiwamo anayedaiwa kutoweka.
Amesema kulikuwa na mkanganyiko na hakuna mbwa aliyepotea.
“Tunataka kuwaambia kuwa mbwa huyo alikuwa kwenye mafunzo ya bwalo la Polisi na mbwa aliyekuwa hayupo siyo hobi,” amesema Mwakalukwa na kuongeza:
“Mbwa wote wapo hakuna hata mmoja aliyetoweka huwa wanaenda kwenye kazi na kurudi.”
 Julai mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alimpa saa saba Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro kuhakikisha mbwa huyo anarudi bandarini baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha.