“Ni ngumu kupata maneno ya kumuelezea Mzee Mkapa, nimemfahamu miaka mingi lakini nimemfahamu zaidi nilipokuwa Katibu CCM Wilaya ya Masasi na yeye alikuwa Mbunge Nanyumbu, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje ila pamoja na ubize aliwatumikia Wananchi” -JK Kikwete

“Wilaya hii ya Masasi ilikuwa na tatizo la njaa wakati ule, nikiwa Katibu CCM Masasi na DC tukabuni mradi wa kilimo cha muhogo hakikupendeza sana kwasababu walikuwa hawapendi sana kula ugali wa mihogo kama Mashemeji zangu Wamakonde, ila Mzee Mkapa alisimama nasi” -JK Kikwete

“Nilipokuwa Rais Mzee Mkapa amenisaidia sana, kuna wakati nikiwa Rais nilipitia changamoto kadhaa, muda mwingine mambo yalikuwa magumu kweli lakini Mzee Mkapa alisimama na mimi “ -JK Kikwete