JKU wa kimataifa, waibuka mabingwa ligi kuu Zanzibar

Klabu ya JKU imeibuka vinara wa ligi kuu ya Zanzibar baada ya kuifunga Jamhuri magoli 3 – 1 na kufikisha alama 33. Magoli mawili ya Salum Mussa katika dakika ya pili na sabini na lile la Posiana Malik katika dakika ya thelathini na sita yalitosha kabisa kuipa JKU ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar mara mbili mfululizo.

Kwa upande wa kisiwani pemba, Zimamoto licha ya kushinda magoli 2 – 1 dhidi ya Opec wameambulia nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 32.

JKU na Zimamoto watawakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa ya CAF. Msimu uliopita pia timu hizi ziliwakilsha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa  lakini wote walitolewa katika hatua za mwanzo.