JKU yaibuka kidedea mchezo wa ngao ya hisani

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar JKU wameibuka kuwa washindi wa mchezo wa ngao ya Hisani baada ya kumfunga klabu ya KMKM kwa mikwaju ya Pelnat 9 kwa 8 mchezo uliopigwa uwanja wa Amani Visiwani Unguja.

Baada ya kumalizika mchezo huo ambao dakika 90 ulimalizwa kwa timu zote zikiwa sare ya moja moja Jku ndio wa kwanza kuandika bao dakika ya 70 lilofungwa na Mborouk Chande kabla ya lile la kurejesha la KMKM dakika ya 87 lilofungwa na Mussa Mbarouk .

Klabu ya Jku imefanikiwa kuchukua rekodi nyengine mpya baada ya kushinda tena ngao ya Hisani mara ya pili mfulilizo Gazeti hili limezugumza na  ,Nohodha Msaidizi wa klabu ya Jku Issa Haidar amesema ni mwanzo mzuri kwa klabu yao kufanya makubwa kwenye msimu huu wa ligi kuu ya Zanzibar unatarajiwa kuanza Oktoba 20 jumamosi hii.

Aidha amewataka wapenzi wanaoiyunga mkono klabu yao waendelee kuipa nafasi na kuiyunga mkono kwenye harakati zao za kusaka vikombe mbali mbali vya ndani na nje ya kimataifa.

Pia  kamati ya mashindano ya ZFA imegawa zawadi kwa washindi mbali mbali ikiwemo Bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar  na ngao ya hisani JKU amekabidhiwa medali ya dhahabu na medali ya Fedha na kiasi cha Tsh Millioni Mbili na Laki Tano kama na Kikombe na ngao ya hisani.

Kwa upande wa Makamo bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar 2017/2018 Zimamoto amekabidhiwa Tsh Millioni moja na nusu kama na medali ya Fedha kama zawadi yake.

Bingwa wa mashindano ya Kombe la FA CUP klabu ya KMKM amekabidhiwa jumla ya Tsh million Moja na mshindi wa pili wa mashindano ya FA Cup klabu ya Jamuhuri amekabidhiwa jumla ya Tsh laki tano .

Kwa upande mwengine taarifa kutoka kwa kamati ya mashindano timu zote hizo zimepata tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2019 mwakani.