jpm

“Tangu SADC ilipoanzishwa hadi sasa Idadi ya Watu imeongezeka kutoka Milion 60 hadi Millon 350 hivi sasa, miundombinu imeimarika, Biashara miongoni mwa Nchi Wanachama imeongezeka kutoka 5% hadi 25%,hali ya maisha na vipato vya Wananchi wetu vimekua,amani na usalama imetawala” Rais JPM

“Tumeboresha pia uchumi ikiwemo kuziimiza Nchi zote zilizopo SADC kuanzisha na kuendeleza viwanda, katika mwaka mmoja uliopita tumesimamia uandaaji wa ajenda za maendeleo ya Jumuiya yetu, katika kipindi cha Uenyekiti wetu tumeandaa dira ya maendeleo ya SADC ya mwaka 2050”

“Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 tumelazimika kufanya mkutano huu kwa njia ya mtandao, nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa wananchi wa Jumuiya hii waliothirika na ugonjwa huu” Rais JPM

“Niwapongeze Nchi wanachama na sekretarieti kwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa wakati wa janga hili, kutokana na miongozo na mikakati mbalimbali iliyotolewa, kwa kiasi kikubwa tumeweza kudhibiti ugonjwa huu kwenye ukanda wetu” – Rais JPM