“Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anajituma kwelikweli, katika suala hili la corona alisimama kweli, kuna wakati nilikuwa namuona kama anasimama peke yake kwenye Wizara” -JPM

“Waziri Ummy sio Proffesional Doctor , unaweza kujiuliza Mwanasiasa anasimama peke yake ila wasaidizi wake ambao Madaktari huoni kitu , kwahiyo nakupongeza sana Waziri Ummy unachapa kazi, umepambana kwelikweli” –JPM

“Nakupongeza sana Ummy najua nilikutesa, sitaki kueleza sana, kwa siku mara nyingine Ummy alikuwa anapigiwa simu zaidi ya mara 8, lakini ndio hivyo, unapokuwa kwenye vita saa nyingine kubembelezana hapana, lakini Ummy unachapa kazi nakupongeza kwelikweli”-JPM .