“Kuna wakati tulipanga sehemu ya kuzika Viongozi iwe Dodoma, Mzee Mkapa akasema nizikeni Lupaso, nilipomuuliza Mzee Kikwete akasema Msoga, nikaogopa kumuuliza Mzee Mwinyi maana ana miaka mingi isije kutokea kitu nikaonekana nimemletea uchuro, mimi pia nataka nizikwe Chato”-JPM

“Baada ya Mkapa kusema akifariki azikwe Lupaso, Kikwete Msoga, mimi nikawaza nikifariki nizikwe Chato, nikasema eneo lililotengwa kwa mazishi ya Viongozi Dodoma labda atazikwa Mzee Malechela tu ambaye kwao Dodoma na hatolimaliza, nikaruhusu eneo litumike kwa mambo mengine”-JPM

“Watu wa Lupaso mna bahati sana kumpata Mzee Mkapa ambaye ni Mzalendo aliyependa nyumbani kwao ndio maana hata akachagua akifariki azikwe Lupaso, nawashukuru wote waliowezesha shughuli za maazishi, leo sina maneno mengi, tumuache Mzee wetu Mkapa apumzike” -Rais Magufuli