“Ilibidi niende Dar es Salaam kwa kutumia Ndege kutokea Mtwara lakini nimepita hii Barabara (Mtwara- Dar es Salaam) makusudi nione hali yake, hii Barabara imeharibika, KM 90 zote zimeharibika. magari yenye uzito mkubwa yameharibu hii Barabara” -Rais Magufuli


“Kazi aliyoifanya Mkapa ameifanya kwa nguvu zote, nawaomba wananchi wa kusini tumuenzi Mkapa kwa kuchapa kazi, tuna eneo zuri mno, ufuta unakubali, mahindi, korosho vyote vinakubali, na mifugo inakubali, tuchape kazi na tupendane, Kero hii ya barabara nimeibeba” Rais Magufuli

“Tumeshalipa zaidi ya Tsh. Bilioni 800 kwa ajili ya korosho, tumemaliza na hii Tsh. Bilioni 20 (iliyotolewa juzi), tuendelee kushikamana na Serikali yetu na tuendelee kuchapa kazi, Mtwara na Lindi ya sasa sio kama ya kipindi cha nyuma, zinapendeza, zinafurahisha” -Rais Magufuli


“Kwa mujibu wa Sheria ya Barabara, Barabara ikishakua ya lami inapata 100% ya ukarabati (Maintanance), Fedha za Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) sijui zinakwenda wapi!, Serikali haijalala, hili la ubovu wa Barabara (Kusini-DSM) nawahakikishia nitalishughulikia mwenyewe” -Rais Magufuli