Mwenyekiti  wa Mkoa wa Magharibi Kichama Mohamed Rajab Said amesema jukumu la Chama Cha Mapinduzi kusimamia Serikali na kutizama kwa ukaribu kabisa mwenendo na maadili  ya Viongozi.

Alisema ili kutimiza kwa vitendo kauli ya Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi DR John Pombe Magufuli na Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein pia na Katibu Mkuu wa wa CCM Dr Bashiru na Dr Mabodi kwa Zanzibar ambao kila siku walikuwa wakiwaasa na kuhimiza viongozi wa chama wawe waadilifu .

Akizungumza  na waandishi wa Habari huko Mwera kwenye ukumbi wa CCM  Mkoa wa Magharibi A kwenye mkutano wa Azimio la kikao cha kamati ya siasa ya Mkoa kuhusu tuhuma alizozitoa Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Mh Nadir.

Akitoa ufafanuzi juu ya mchango uliotolewa mbele ya Baraza la Wawakilishi na Mh Nadir kuhusu tuhuma nzito za uzushi zilizotolewa kwa mwenzetu wa kamati ya siasa Mkoa Magharibi kichama  ambapo sio kweli wala uthibitisho hakuna.

Hivyo Mwenyekiti alisema anaomba chama kichukuwe hatua zinazofaa baada ya kujiridhisha kwa tuhuma hizo na ikithibitika sheria ichukuwe kuanzia tawi hadi uongozi wa juu.

Alisema kiwanja hicho alipewa mjumbe huyo kisheria na vielelezo vyote vipo ikiwa kama ni fidia  ambapo kiwanja hicho kipo Mbweni kwani serikali haitoi ardhi kwa mwenye nguvu bali kinatoa kisheria.