Jukwaa la wahariri nchini walaani vitendo vinavyofanywa Jeshi la Polisi dhidi ya waandishi wa habari pindi wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kupigwa kwa waandishi wawili siku ya Jumatano tarehe  8, Agosti ambapo mwandishi kutoka wilayani Tarime mkoani Sita Tuma aliyekuwa akitekeleza majukumu yake wakati jeshi hilo lilipowatawanya kwa silaha za moto wafuasi wa CHADEMA waliokuwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.

Akizungumza na East Africa Radio, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Dodatus Balile amesema kuwa kitendo hicho cha kukamatwa kwa mwandishi na kushikiliwa wakati akiwa kazini si sahihi na taratibu za mamlaka haziruhusu vitendo dhidi ya wanahabari.

“Mwandishi amekamatwa akiwa kwenye eneo la kazi wala hakufika pale kwaajili ya kuandamana kama walivyodai wao, kama wao walivyokuwa kazini hata sisi tunakuwa kazini”, amesema Balile.

Tarehe 8, Agosti Jeshi la polisi , wilayani Tarime mkoani Mara, liliwashikilia Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko, mwandishi wa habari, pamoja na mara baada ya kuamuru wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), kusitisha kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea nchini.

Sanjari na hayo Shirikisho la soka nchini (TFF) pia limelaani kitendo cha mwandishi wa habari za michezo kupigwa na maaskari waliokuwa uwanjani hapo wakati akitekeleza majukumu yake siku ya sherehe za Simba Day, ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewataka TFF  kuweka utaratibu mzuri kwa waandishi wa habari kuweza kufanya kazi zao vyema wanapokuwa uwanjani bila kusuguana na vyombo vya ulinzi.