Wanafunzi Wametakiwa Kusoma Kwa  Bidii Na  Kuzingatia Masomo  Yao   Wakati  Wakiwa  Masomoni

Yamesemwa hayo na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Chuo Cha Mwalim Nyerere Dr;  Steven Wasira Katika Mahafali Ya Nne Ya Chuo Cha Kumbukumbu Ya Mwalimu Nyerere Kampas  Ya  Karume Zanzibar Amewataka Wanafunzi Kuzingatia Wanachosomeshwa Na Kuwa Na Uweledi Ili Wawe Wataalam  Wazuri Hapa  Nchini

Kwa Upande Wake Mkuu Wa Chuo Dr;Shadrak Mwakalila Amesema  Wamepata Mafanikio Makubwa  Kutokana Na Kuwa Na Mashirikiano  Walionayo Kutoka Kwa Ngazi Ya Masheha,Mkoa,Taifa Na Serikali Ya  Mapinduzi Ya  Zanzibar Na  Wanatarajia  Ifiikapo Mwaka 2020 Kuanzisha Tawi Jipya Huko Kisiwani Pemba ikiwa Lengo Ni Kuongeza Wataalamu Wenye Sifa Bora Nchini

Licha Ya Mafanikio Waliopata Aidha Wanakabiliwa  Na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo  Ukosefu Wa Fedha Za Maendeleo Ambazo Zingeweza  Kusaidia Kuleta  Maendeleo Ya Chuo Hicho,Upungufu Wa Wafanyakazi ,Kukosekana Kwa Mabweni ya Wanafunzi Wanaokuja Kutoka Sehemu  Za Mbali Na  Chuo,Kujaa Maji Pembezoni Mwa Chuo Hicho wakati wa mvua

Jumla  Ya Wanafunzi 1753 Wa Chuo Hicho Wamehitimu Masomo Yao Kwa Ngazi Ya Astashada,Shahada Na Stashahada