Wastaafu wanaopokelea pencheni zao katika mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wamewaomba mfuko huo kuwaongea posho ili kujikimu kimaisha .

Ombi Hilo wamelitoa huko Kitogani katika ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Kusini wakati wa muendelezo wa zoezi la uhakiki kwa wastaafu wanaopokea pencheni zao katika mfuko huo ambapo wamesema kwasasa mahitaji yameongezeka tofautina zamazamani. 

Wakizungumzia swala la kupunguziwa masafa ya kutoka shamba kwenda mjini wameipongeza ZSSF kwa kuwarahisishia huduma hio ambapo zoezi Hilo litakuwa kwa siku 3 kwenye Wilaya hio.

Kwaupande wake afisa habari na masoko muandamizi kutoka ZSSF Raya Hamdani Khamis amesema wamelipokea ombi hilo na wanalifanyia kazi na hali ikiruhusu Basi watawaongeza posho wastaafu hao.


Aidha Bi Raya amewakumbusha wastaafu ambao hawajajihakiki taarifa zao kwenda vituoni na kujihakiki.

Zoezi la uhakiki kwa wastaafu wanaopokea pencheni zao katika mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF linalofanyika kila baada ya miezi 6 ya kila mwaka hadi sasa jumla ya wastaafu 8,328 wameshahakiki taarifa zao kutoka vitoa tofauti kwa upande wa Zanzibar ambapo jumla ya wastaafu 11,100 wanatarajiwa kuhakikiwa taarifa zao nchini.