Waziri wa Kilimo, Mali Asili, Mifugo na Uvuvi Mmanga Mjengo Mjawiri ameitaka jumuiya Mabaraza ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kushirikiana vyema na Serekali katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Ameyasema hayo leo wakati akizindua jumuiya hio hafla iliyofanyika huko katika Ukumbi wa Hotel ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar amesema serekali itahakikisha na kuona wanapatiwa huduma ambazo zitawezakuwasaidia na kuwatatulia changamoto zao ilikuweza kufanikiwa kwa urahisi.

Akisoma risala Mshika fedha wa Jumuiya hiyo Hadia Ali Makame amesema licha ya jitihada zilizokuwepo katika jumuiya hio ila zipo changamoto wanazokabiliana kama kukosa barua ya Sheha kwa wepesi katika usafirishaji wa mazao yao na pia masuala ya internet na komputa.

Aidha Hadia ameiomba serekali kuwasaidia vyombo vya usafiri, kuwashirikisha katika ungawaji wa pembejeo pamoja na kuwapatia mfuko wa Bank kwa kuwakopesha wakulima kwa unafuu.

Jumuiya ya Mabaraza ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Zanzibar imeanzishwa mwaka 2019 ikiwa na lengo la kusaidia jamii katika maendeleo endelevu ya uchumi Zanzibar.

Na…Rauhiya Mussa Shaaban