Uongozi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Zanzibar imesema itaendelea kutoa elimu ya Dini  kwa vijana kwa lengo la kuwajengea vijana misingi ya Dini ya kiislamu ili kuwa na Taifa lenye maadili mema.

Alisema kwa sasa jamii  kuwa inakabiliwa na changamoto ya kukosa maadili yaliyo mema ambapo husababisha kutokuwa na Ustaw uliomzuri.

Kauli hiyo imetolewa na Sheikh Ali Bin wakati wa kupokea zawadi za washindi wa Mashindo ya Quran zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Ayoub Mohamed Mahoumd,

Hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo zimefanyika katika ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa Vuga Mjini Magharib Unguja.

Sheikh Ali Bin Jumuiya yao itaendelea na harakati za kutoa elimu kwa vijana mbalimbali ndani na nje ya Zanzibar kwa lengo la kujenga ustawi bora kwa vijana Nchini.

“Hivi sasa jamii inakabiliwa na tatizo la kutokuwa na maadili mema jambo amblo huzorotesha ukuaji wa ustawi wa jamii katika nchi hivyo sisi kama Jumuiya ya kuhifadhisha qurani tunaendelea kutoa elimu hii ili kusadia kujenga jamii hii inayoonekana kuharibika” alisema Sheikh huyo.

Aliongeza kusema kuwa mbali na kujenga ustawi wa jamii jumuiya hiyo itajitahidi kutoa elimu hiyo ili kufikia malengo ya kushika kitabu cha mwenyezimungu kwa kila mzanzibar na mtanzania muislamu.

Akizungumzia suala la zawadi hizo za laptop zilizotolewa na mkuu wa mkoa wa mjini magharib unguja alimpongeza mkuu huyo wa mkoa na kuomba kuendelea na jihudi hizo za kuwasaidia na kuwapongeza wanajamii wanapofanya vizuri.

Nae Mkuu wa MKoa wa Mjini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud alisema ni faraja ilioje kuona vijana wamehifadhi vyema quran na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono ili kuimarisha umoja na upendo baina ya wananchi wake.

Aidha  Ayoub alisema serikali ya Mkoa itaendelea na utamaduni huo wa kuwapokea vijana hao ili kuunga mkono na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya katika kuitangaza Zanzibar katika mataifa mbali mbali.

hata hivyo  Mkuu wa Mkoa huyo alisisitiza kuendelea  kusimamia sheria, taratibu na miongozo ya nchi katika kuongoza wananchi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuondosha vitendo vinavyopelekea mmong’onyoko wa maadili ili kuendelea kuwa na jamii yenye maadili.

Washindi wawili wa mashindano ya Quran  akiwemo Masoud Khamis Sultan aliyeshika nafasi ya pili katika mashindano yaliyofanyika nchini kenya  amekabidhiwa shilingi milioni moja na laki tatu sambamba na kompyuta  na Shamis  Mwalim Said akikabidhiwa shilingi milioni moja na kompyuta  akishika nafasi ya  tatu katika mashindano yaliyofanyika jijini dar es slamaa.

Zawadi zilizotolewa na mkuu huyo ni pamoja na laptop na Shiling Milion mbili na laki tatu.