Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kuacha tabia ya kupakia mtoto zaidi ya mmoja kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Akizungumza na hits fm Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Pemba Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa kusini Pemba Hassan Nassir Ali amesema kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani vyombo vya maringi mawili vinatakiwa kupanda watu wawili pekee na sio zaidi.

Amesema kwa sasa baadhi ya wananchi wanatabia ya kuwapakiwa watoto wao zaidi ya mmoja kuwapeleka skuli jambo ambalo ni kosa kisheria na linaweza kuhatarisha usalama wao.

Kamanda Nassir amesema kutokana na hali hiyo yeyote atakaebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumziaoperesheni za usalama barabaraniKamanda Nassir amesema wamefanikiwa kuvikamata vyombo vya maringi mawili 56 kutokana na makosa tofauti ikiwemo mwendo kasi na kutokuwa na lesseni.

Aidha Kamanda Nassir amesema jeshi la polisi litaendelea na operesheni ili kuhakikisha hali ya usalama barabarani inaimarika zaidi.

 Rauhiya Mussa Shaaban