Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kaskazini “A” OCD Mussa Khamis Mussa amelitaka shirikisho la michenzo Zanzibar kufanya ushawishi katika kutetea haki za Viziwi kwa mujibu wa sheria za nchi  zilivyo ili kujiepusha kuingia katika migogoro. 

Akifungua  mafunzo kwa jeshi la  Polisi yaliyoandaliwa na shirikisho hilo huko Katika ukumbi wa chuo cha mafunzo ya amali Mkokotoni  kwa niaba ya kamanda wa Wilaya hiyo Msaidizi kamanda wa polisi Yussuf Mussa Juma amesema sheria ni kitu pekee  kitakachoweza kuwasaidia wananchi hususani viziwi kupatiwa haki zao kwani kila jambo lina sheria take ambazo hakuna wa kuzipiga na hufuatwa kwa mujibu wa sheria. 

Amesema jeshi la  polisi  lipotayari kushirikiana na shirikisho katika kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu wakiwemo viziwi ili kuona kila mmoja analindiwa heshima wake. 

Amesisitiza kuwa mafunzo yanayotolewa  kwa shirikisho yaendane na utekeleza katika harakati za utetezi na ushawishi ili jamii ya viziwi iweze kutendewa haki zao kuanzia hatua za mawasiliano hadi kwenye upatikanaji wa haki  zao za msingi. 

Kwaupande wake Mratibu wa shirikisho hilo Jide Khamis ameiyomba serikali iyajiri wakalimani hasa  katika maeneo muhimu ikiwemo mahkaman, Magereza, hospital ili kusaidia upatikanaji wa haki pamoja na kurahisisha mawasiliano. 

Amesema bado jamii ya viziwi haitendewi haki kisheria katika jamii kutokana bado mikataba ya kisheria kutokufanyiwa kazi na jamii kuweza kuitambua baada ya nchi  kuiridhia. 

Nao baadhi ya Askari Polisi waliopatiwa mafunzo akiwemo Mtumwa Haji Shaka na Juma Omar Hamad wameahidi kushirikiana na jamii ya watu wenye  ulemavu ili  kuhakikisha wanatendewa haki kwa mujibu wa sheria.