Jumla ya waamuzi 40 wanatarajia kushiriki kwenye kozi ya utimamu wa mwili (COPA TEST) inayotarajia kufanyika ijumaa tarehe 12/2018 kwa ajili ya mandalizi ya Ligi kuu ya Zanzibar na ligi nyengine zinazondaliwa na ZFA Taifa.

Akizugumza na Zanzibar24 Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Zanzibar Muhsin Ali Kamara amesema zoezi hilo limepelekwa mbele baada ya tarehe kumi baada ya matatizo ya kiwanja cha Amani.

Amesema mafunzo hayo yataanza na  vipimo vya Afya kwa waamuzi wote siku ya Alhamisi kabla ya kuja uwanjani kwa siku ya ijumaa kwa ajili ya mafunzo yenyewe, aidha amesema mafunzo hayo yataendana na semina maalum kwa ajili ya mabadiliko ya sheria za mpira wa miguu kwa muda wa siku mbili .

Kwa upande mwengine Mzee kamara amesema kozi hiyo inatarajia kufanyika Uwanja wa Amani majira ya Asubuhi na itashirikisha waamuzi kutoka unguja na Pemba, na ameelezea msimu uliopita walikuwa wanachangamoto ya waamuzi wengi umri wao ulifika kikomo hivyo darasa hilo litakuwa mchujo kwa baadhi ya waamuzi.

Pia amesema wao kama Kamati ya waamuzi Zanzibar wamejipanga kuhakikisha wanakuwa na waamuzi wengi vijana licha ya kuwa darasa maalum la waamuzi vijana ila mipango yao kuwashawishi taasisi mbali mbali kuja kuleta waamuzi vijana kupatiwa mafunzo ya waamuzi.

Aidha amesema wamewaalika waamuzi kutoka kwenye wilaya zote   ili kutafuta waamuzi wengi vijana na inaweza kusabiabisha kuwa na waamuzi wengi zaidi.

‘’Mafunzo yetu haya yanatarajia kusimamia wenyewe tunao wakufunzi wengi sana wamesoma kozi za Kimataifa hivyo hii ni ligi ya ndani hivyo tutasimamia wenyewe’’ Alimalizia Mushin Kamara.