Kampuni ya China inayojulikana kama ENGO Holdings Limited imeanza kujenga kiwanda cha kutengeneza kompyuta na simu za mkononi nchini Uganda. Kiwanda hicho kinajengwa katika eneo la kibiashara la Namanye nchini humo.

Pindi kiwanda hicho kitakapokamilika kitakuwa cha kwanza nchini humo. Tayari kampuni hiyo imesaini makubaliano na mamlaka ya kitaifa ya Technolojia kwa niaba ya serikali.

Waziri wa Mawasiliano wa Uganda amesema kiwanda hicho kitaunda ajira nyingi kwa waganda wengi ambao wengi wao hawana kazi. Taarifa hii inakuja miezi michache tu baada ya kampuni nyingine ya kutengeneza simu ya China kufungua kiwanda cha kuunganisha simu nchini humo.