WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la polisi nchini kutoruhusu Vyama vya siasa kufanya mikutano ya Hadhara.

Amesema kuna baadhi ya Vyama vya siasa vinafanya Mikutano ya hadhara Mikusanyiko ya siasa jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Hayo yamebainishwa wakati akizungumza na Wananchi katika kiwanja cha kombawapya Mjini Zanzibar wakati akisikiliza kero za wanachi zilizopo katika mkoa huo.

Amesema huu si wakati wa Vyama vya siasa kufanya mikutano ya kutambulisha vyama vyao na kunadi sera zao badala  yake wajikite katika shughuli za maendeleo.

Amesema kufanya mikutano ya hadhara ni kurejesha nyuma shughuli za maendeleo ambazo wanatakiwa kufanya wananchi ili kujiiingizia kipato na kuimarisha uchumi wa nchi.

Alisema wakati umefika kwa Jeshi la polisi kutokivumilia Chama chochote ambacho kitakiuka agizo la serikali juu ya kuendeleza mikutano ya hadhara ambayo inaendelezwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa Zanzibar.

’’naliagiza jeshi la polisi Zanzibar kupitia kwa kamishna wake kushughulikia chama chochote cha siasa ambacho kitafanya mikutano ya hadhara na kutishia amani ya Nchi,wakati wa kufanya mikutano haujafika’’. Alisema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri Kangi amechukua fursa hiyo kukemea suala la Baadhi ya watendaji wa jeshi la Polisi kufanya kazi kinyume na utaratibu ikiwemo kushirikiana na Wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya Nchini.

Amesema serikali imekuwa ikipambana kwa kiasi kikubwa kutokomeza sula la madawa ya kulevya lakini bado baadhi ya Watendaji wa jeshi la polisi wamekuwa wakirejesha nyuma jitihada hizo.

   Awali akizungumzia suala la amani Nchini Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Masauni amesema Hali ya Amani na Utulivu katika Mkoa huo ni Nzuri jambo ambalo linachnagia ukuwaji wa uchumi Nchini.

Amesema kuna baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikijaribu kuvyunja amani kwa kuandaa mikutano kinyume na sheria lakini Jeshi la polisi litahakikisha linadhibiti mikutano hiyo ili kuiendeleza kuna baadhi ya Vyama vya siasa vimekuwa vinaanza kuharibu amani kwa kufanya mikutano yao kinyume amani iliopo.

Akizungumzia suala la Udhalilishaji wa kijinsia Masauni amesema bado tatizo la udhalilishaji limekuwa tatizo kutokana na baadhi ya Wananchi kutokubali kutoa ushahidi wakati kesi  zikisikilizwa sehemu husika.

Amesema wakati umefika kwa wananchi kuthamini juhudi za serikali katika kupambana na tatizo la Udhalilishaji wa wanawake na watoto ili kutokomeza tatizo hilo Nchini.

Katika mkutano huo Waziri huyo alipata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Mjini Magharib  Unguja na kuahidi kuzitatua haraka ili wananchi waweze kunufaika na haki zao za msingi kikatiba.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.