Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali inatarajia kupeleka Kanuni Bungeni ili kuwabana Wamiliki wa nyumba wanaowalazimisha Wapangaji kulipa kodi kwa muda wa miezi 6 hadi 12.

Amesema, siyo sawa kwa Mmiliki wa nyumba kumlazimisha Mpangaji wake kulipa kodi ya miezi sita au mwaka, japokuwa suala la makubaliano ya upangaji ni la watu wawili.

Ametoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge Nape Nnauye kutaka majibu ya Serikali kuhusu Wamiliki wa nyumba wanaolazimisha kodi ya miezi sita au mwaka na kuishauri Serikali kuweka sheria ya malipo ya mwezi mmoja