Katibu wa Chadema Jimbo la Manyoni Mashariki, Alex Jonas amekutwa barabarani akiwa na majeraha yanayoonyesha amechomwa na kitu chenye ncha kali.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa amesema kuwa tukio hilo lipo na kwamba bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.

“Ni kweli kuna tukio la Katibu wa Chadema Wilaya ya Manyoni kukutwa amefariki dunia leo asubuhi, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kutoa taarifa kamili,”amesema.

Mwangisa amesema yeye yupo kwenye kikao mkoani Singida lakini taarifa hizo amezipata na kwamba baadaye watatoa taarifa zaidi ya tukio hilo.