Tukio la kutekwa nyara kwa Mfanyabiashara maarufu nchini MO Dewji limemuibua Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba.

Waziri January Makamba ameandika katika Twitter yake kuwa “Nimezungumza na baba yake @moodewji. Habari za kutekwa kwa rafiki yetu Mo ni za kweli. Nimetikiswa sana. Naamini polisi watatoa taarifa kamili. Mohammed ana familia na watoto wadogo. Tumuombee yeye na familia yake. Tusaidie kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.