JESHI la polisi Zanzibar limesema kuwa litafanya uchunguzi wa kifo cha aliekuwa  naibu kamishna wa jeshi hilo, ACP Azizi Juma Mohammed aliefariki dunia usiku wa kuamkia jana.

Marehemu Azizi alikutwa akiwa ameshafariki nje ya nyumba yake huku akiwa amefungwa kamba.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia June 9,2019  huko Kibweni wilayani ya Magharib “A” Mkoa wa Mjini MAGHARIBI Unguja.

Akizungumza mara baada ya mazishi Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar Mohammed Haji Hassan amesema sio Jambo la kawaida kuona Askari wake akifa katika mazingira yenye utata.

Alisema sio suala zuri na jema kuona vifo vya aina hii vikitokea Kwa watendaji wa jeshi la polisi na huku sababu hasa ikishindwa kutambulika.

” Tunatia wasisi mkubwa Sana kuhusu vifo vya aina hii vinatuweka katika wakati mgumu ambao bado unazidi kutupa mashaka”.

Aidha alisema jeshi la polisi limepata pengo kubwa Sana kwani Marehem alikuwa na mchango mkubwa Sana wakati wa uhai wake, kwani mbali ya kufanya akzi zake za kawaidi pia alikuwa Mwalimu wa jeshi hilo.

Nae naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Hamad Yussuf Massaun alisema jeshi limepoteza kamanda ambae ni tegemeo kwa wananchi na taifa.