Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yeye hawezi kumhukumu Lowassa kwa uamuzi wake wa kuondoka upinzani na kurudi CCM ingawa anakiri amewaumiza na kuwaangusha wapinzani kwa uamuzi wake huo

Amefafanua kuwa Lowassa ni tofauti na yeye kwakuwa yeye ameweza kuvumilia mikikimikiki na matokeo ya kuwa mpinzani ila Lowassa alitoka kuwa Waziri Mkuu na kuna mambo aliyategemea Upinzani lakini hali ikawa tofauti na matarajio

“Na ninavyosikia mimi familia yake ilimshinikiza, kwamba kuna mmoja kati ya wakwe zake alikuwa gerezani na watoto wake walikuwa wanamwambia ‘baba unaona… ndugu yetu sisi anapata shida kwa sababu wewe uko upinzani.’ Kwahiyo, lile shinikizo la familia lilikuwa kubwa sana” alisema maalim Seif