Afisa Mkuu wa Polisi, Sabina Kerubo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mwandishi wa Habari wa The Star Bw. Eric Oloo kutokana na mwili wa marehemu kukutwa nyumbani kwake mnamo Novemba 21

Afisa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Siaya, James On’gondo ambaye aliamuru kuwa Afisa huyo aendelee kuwa kizuizini Kituo cha Polisi cha Siaya kwa siku 14

Katika hati ya kiapo, wapelelezi wanaoshughulikia kesi hiyo wameomba muda wa nyongeza wa kumshikilia Afisa huyo ili kumaliza uchunguzi juu ya mauaji hayo

Aidha, wiki mbili zilizopita Mahakama iliamuru ndugu wawili, Victor Ogola Luta na Franklin Joel Luta, kukamatwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa tena mnamo tarehe 10 Desemba mwaka huu