Kikosi cha Taifa Stars kimpoteza tena mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika awamu hii dhidi ya Kenya kwa kuchapwa mabao 3-2.

Kipigo hiki kimekuwa cha pili baada ya mechi ya kwanza kufungwa mabao 2-0 na Senegal.

Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga aliyeingia kambani mara mbili huku moja likiwekwa kambani na Johanna Omolo.

Taifa Stars imefunga mabao yake kupitia kwa Mbwana Samatta na Simon Msuva

Tanzania ilitangulia kuchukua uongozi katika dakika ya sita ya mchezo kupitia mshambuliaji Simon Msuva aliyemalizia shambulio kali lililoanzia kwa nahodha Mbwana Samatta.

Samatta

Michael Olunga akaisawazishia Kenya katika dakika 39 kwa bao safi la tiki taka, lakini dakika mbili baadaye, nahodha wa Tanzania akairudishia timu yake uongozi katika dakika ya 41 baada ya kuipangua safu ya ulinzi ya Kenya.

Kipindi cha kwanza kikaisha kwa Tanzania kuwa kifua mbele kwa goli 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, huku safu ya kiungo ya Kenya ikiongozwa na nahodha Victor Wanyama ikiutawala mchezo huo.

Kenya pia ilionekana dhahri kuwashinda Tanzania katika kucheza mipira ya juu.

Johanna Omollo aliirudisha Kenya mchezoni katika dakika ya 62 kwa kupiga kichwa kikali katika eneo la hatari la Tanzania bila kubughudhiwa na walinzi wa Tanzania.

Baada ya hapo Kenya waendelea kulisakama lango la Tanzania, na ilikuwa ni Michael Olunga tena ambaye aliizamisha Tanzania kwa kufunga goli lake la pili na la tatu kwa Kenya katika dakika ya 80.

Olunga ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.

Ujumbe wa Twitter wa @RailaOdinga: What a splendid performance #HarambeeStars coupled with great composure coming from behind twice to deservedly win the game. Bravo! Kenyans are firmly rooting for you. All the best as you continue striving to qualify for the #AFCON2019 round of 16. Hongera