Wizara ya Afya nchini Kenya imepiga marufuku maduka ya dawa na wakemia kuuza dawa za Chloroquine na Hydroxychloroquine kwa watu wasio na kibali cha kutumia dawa hizo kutoka kwa Daktari.

Agizo hilo linakuja baada ya watu nchini humo kuanza kununua dawa hizo kwa wingi kufuatia madai kuwa zinaweza kutibu corona baada ya visa vya Corona kuongezeka nchini humo.

Wiki chache zilizopita Rais wa Marekani Donald Trump alidai Chloroquine inaweza kuwa tiba ya corona kauli ambayo imepelekea uhitaji mkubwa wa dawa hiyo Marekani na nchi nyingine.

Hata hivyo, wataalamu wa afya bado hawajaruhusu vidonge hivyo kutumika kwa ajili ya kutibu Virusi vya Covid 19.