Kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha inayowakabili waliokuwa askari polisi wanane mkoani Mwanza, inaanza kusikilizwa leo kwa mara ya kwanza, katika mahakama ya hakimu mkazi Mwanza.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2019 inasikilizwa na hakimu mkazi mfawidhi Rhoda Ngimilanga.

Washitakiwa wanne katika kesi hiyo ambao ni wafanyabiashara wa madini ya dhahabu walikiri makosa yao na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela au kulipa faini ya zaidi ya shilingi milioni 500.

Hata hivyo walilipa faini na kuachiliwa huru, huku madini yenye thamani ya shilingi bilioni 27, magari mawili, mzani wa kupimia dhahabu na fedha taslimu shilingi milioni 305 zikitaifishwa na serikali.