Kesi ya uchochezi inayomkabili Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu leo Julai 30, 2020, imeahirishwa hadi Agosti 26, baada ya mtuhumiwa kushindwa kufika katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.


Wakili Peter Kibatala, ameomba tarehe nyingine na kuieleza Mahakama kuwa Lissu alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu na alishauriwa kupumzika kutokana na hali yake ili awaze kuangalia afya yake

Mawakali wa Jamhuri hawakuweka pingamizi na kesi zote 2, namba 123 ya 2017 (Anayodaiwa kutoa maneno ya kuumiza hisia za Kidini) na namba 236 ya mwaka 2017 (Anayodaiwa kutoa maneno ya Kichochezi) zimeahirishwa hadi Agosti 26 mwaka huu