Mdhamini wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bw. Pandu Ameir Kificho amesema maendeleeo ya nchi yaliopatikana yanatokana na Sera madhubuti zilizowekwa na Viongozi wa Chama hicho.

Amesema Chama hicho kipo Imara kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi hivyo ni vyema kukiunga mkono ili kizidi kuimarika na kuendelea kushika Dola.

Ameyasema hayo huko Amani CCM Mkoa wakati alipokuwa akizungumzia miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

Bw. Kificho ambae pia ni Spika Mstafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar amewahakikishia Wananchi kuwa Chama hicho kitaendelea kusimamia mipango ya Serikali ili kuhakikisha Wananchi wa Mjini na Vijijini Wanapata huduma bila Ubaguzi.

Hata hivyo Bw. Kificho amewataka Viongozi waliochagulkiwa kushuka chini kwa Wananchi ili kuweza kubaini matatizo yanayowakabili na kuyapatia ufumbuzi Kwa muda muafaka na kuwafanya kuzidi kujenga imani na Chama hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Muhammed Mahmoud amesema ili kuhakikisha wanaunga Mkono Juhudi za Waasisi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi wanatarajia kuandaa Kongamano maalum litakaloelezea Mchango mkubwa uliotolewa na Waasisi hao.