Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba, amehoji juu ya matumizi ya Sh. bilioni 4 alizotumia mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ kulipa mishahara.

Hiyo imekuja kufuatia mwekezaji huyo kuamua kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, muda mfupi baada ya Simba kufungwa na Mtibwa Sugar katika fainali ya Mapinduzi Cup kisiwani Zanzibar jana, Januari 13.

Dkt. Kingwangalla amehoji kuwa hizo bilioni nne ambazo Mo amelipa kama mishahara ndani ya klabu hiyo zimefanyika kwa makubaliano gani na kwa kujiondoa kwake katika nafasi hiyo, mishahara itaendelea kulipwaje?.

Dr. Kigwangalla, H.@HKigwangalla

Poleni wanasimba wenzangu, ‘kisukari kimetuvuruga’, hivi kuna mtu anaweza kunisaidia? Hii mishahara ya 4bn iliyolipwa na Mo inalipwa kwa makubaliano gani? Isijekuwa ndiyo katika ile 20bn ya manunuzi ya hisa 50%, ama manunuzi yalikwishafanyika? Anavyojitoa, italipwaje? #NguvuMoja6387:38 AM – Jan 14, 2020Twitter Ads info and privacy209 people are talking about this

Baada ya mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup kumalizika kwa Simba kupoteza kwa bao moja mbele ya Mtibwa Sugar, bilionea Mo Dewji akaandika katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe kuwa hatoendelea na nafasi yake, atabakia kama mwekezaji na nguvu kubwa ataiwekeza kwenye miundombinu na soka la vijana.

Mohammed Dewji MO@moodewji

It’s a pity simba couldn’t win. After paying salaries of close to 4 billion a year. I resign as the chair of the board and will remain as an investor. Simba Nguvu moja. I will focus on developing infrastructure and a youth academy!5,76910:10 PM – Jan 13, 2020Twitter Ads info and privacy2,911 people are talking about this