Kijana adaiwa kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile bila ridhaa

 Mwanaume mmoja mkoani Kigoma anayefahamika kwa jina la Teleza, ametajwa kuwaingilia watu  hasa wanawake ambao hawajaolewa nyakati za usiku wa manane na kufanya nao mapenzi bila ya ridhaa yao.

Kwa mujibu wa madai yaliyotolewa na baadhi ya wananchi mkoani humo, bwana huyo amekuwa akiwaingilia ndani ya nyumba zao hasa zinapofika nyakati za usiku wa manane ambapo huwalazimisha kuwaingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yao.

Wananchi hao wamedai kuwa  mwanzoni walidhani vitendo hivyo vinasababaishwa na imani za kishirikina ambapo amekuwa akiwafuata wanawake ambao hawana waume zao hali ambayo inayawafanya washindwe kutoka nje nyakati za usiku.

Akizungumzia juu ya vitendo hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga amesema hajawahi kupata taarifa yoyote juu ya uwepo wa mtu huyo lakini ameahidi kufuatilia ili kuhakikisha anapatikana ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kifupi wala simjui, na wala sijawahi kusikia ila kama yupo kweli hivyo ni vitendo vya kihuni, tutahakikisha tunamkata ili afike kwenye vyombo vya sheria ili kujibu madai yake kwa hiyo niwahakikishie wananchi Teleza atakamatwa.”