Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Manchali, Mizengo Chilatu (28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi, huku chanzo cha tukio hilo kikitajwa kuwa ni ulevi wa kupindukia na imani za kishirikina.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Giles Muroto ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dodoma ambapo mbali na tukio hilo, Watu wengine wanne katika nyakati tofauti tofauti wamekamatwa kwa makosa kama hayo ya ubakaji.