Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Suleiman anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 17 hadi 19 amefariki dunia majira ya saa 12 jioni leo katika pwani ya Coconut Chukwani.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kijana huyo aliyekuwa ameongozana na mwenzake amefikwa na umauti wakati akiogelea katika pwani hiyo na ndipo ghafla wenzake wakawa hawamuoni. Baada ya kutafutwa kwa muda alikutwa ndani ya maji akiwa amekwisha fariki.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni Daktari alithibitisha kufariki kwa kijana huyo baada ya kumkagua mwilini mwake.

Suleiman (Kulia) kabla ya kufikwa na umauti

Mama mdogo wa Marehemu Bi. Asma Juma amesema marehemu Suleiman ni mkazi wa Dar es Salaam na alikuja Zanzibar kwa ajili ya masomo.

Mwili wa Marehemu umepokelewa katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa uchunguzi zaidi.