Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Ahmada Makame Mtumweni mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa Kidiko Pungwe amefariki Dunia baada ya kuzidiwa na maji wakati akifata Ngalawa kwa ajili ya kwenda kuvua.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Haji Abdallah Haji amesema tukio hilo limetokea 16-05-2019 majira ya alfajiri huko Kidiko Pungwe Bumbwini.

Amemtaja Marehemu huyo kuwa Ahamada Makame Mtumweni maiti yake imefikishwa katika hospitali ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi na kukabidhiwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi.

Kamanda Haji ametoa wito kwa jamii wawe makini pindi pale wanapokwenda pwani kwa ajili ya kuvua na pia kufahamu utabiri wa hali ya hewa ili kuepusha vifo visivyo vya lazima  na kuwataka kujua kuwa kipindi  hichi cha upepo mkubwa hivyo nikutambua hali hiyo.


Rauhiya Mussa Shaaban