Abdul-Samadu Shafii Abdalla mwenye umri wa miaka 20 Mkaazi wa Miembeni Mjini Unguja amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati akiogelea huko Kizimkazi Dimbani Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea Jana majira ya saa kumi na moja jioni huko pwani ya Kizimkaz Dimbani .

Ameongeza kusema kuwa mwili wa marehemu umefikishwa  hospital ya cottage kwa unhunguzi baada ya kukamilika wamekabidhiwa jamaa zake kwa mazishi huku kifo chake kimesababishwa kwa kukosa hewa baada ya kuzama.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Kusini Abdul -azizi Hamad Ibrahimu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watahakikisha wanaweka ulinzi kwa ajili ya wageni pamoja na wenyeji pindi pale wanapofika katika fukwe za bahari.

Nae Sheha wa shehia hiyo Kassimu Ibrahim Yahya amekiri kuwepo kwa  tukio hilo na kusema kuwa wameufikisha mwili marehemu katika hospital ya cottage makunduchi na kuwapa taarifa wazazi wake ilikuutambua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya mazishi.

Sambamba na hayo Kamanda Suleiman amewataka wageni na wenyeji kuwa makini pindi pale wanapokuwa katika fukwe za bahari na kuhakikisha wanatambua kuogelea pale wanapoingia katika bahari za fukwe.

Rauhiya Mussa Shaaban