Kijiji cha Uzi chapatwa na simanzi ndani ya mkesha wa mwaka mpya 2019

Mtu mmoja akitambulika kwajina Zahor Abdalla  Mohd (25)  mkaazi wa kijiji cha uzi  shakani wilaya ya kati mkoa wa kusini unguja amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa kuifunga juu ya  muembe huku ikisemekana kuwa ni msongo wa mawazo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja kamishna msaidizi muandamizi Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea tarehe 1-1-2019 majira ya saa 11 :00 alfajiri huko kijiji cha uzi mkoa wa kusini unguja

Kamanda suleiman amefafanua kuhusiana na tukio hilo waliweza kuzugumza na familia ya marehemu kuhusiana na kijana wao na kusema kuwa walitegemea terehe mosi ya jana ya mwezi huu kupeleka mtoto wao katika kituo cha afya cha kidongo chekundu kwa ajili ya matibabu na hatimae kijana huyo amejinyonga

Marehemu amefanyiwa uchunguzi katika hospitali ya mnazimmoja na kukabidhiwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi

Sambamba na hayo kamanda suleiman  ametoa wito kwa jamii kuwa karibu na vijana wao ilikutambua changamoto zao na kuweza kuepuka athari mbaya inayoweza kujitokeza kwao.

Rauhiya mussa shaaban