Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 20  Salum Ali Haji, ametangaza kikosi cha  awali cha wachezaji 38, kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Cecafa ya Vijana yanayotarajiwa kufanyika Uganda Disemba 15-25, 2018 .

Kocha Salum ametangaza kikosi hicho kwenye Ukumbi wa uwanja wa Amaan , katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mchana wa leo.

Walioitwa kuunda kikosi hicho upande wa Makipa yupo, Peter Dotto Mashauri (Black Sailors), Abdulattif Said Masoud (Jamhuri), Mwinyi Ali Mwinyi (Mapembeani) na Yakoub Suleiman (Muembeladu).

Mabeki: Khalid Khamis (Simba FC ya Zanzibar), Abdul hamid Ramadhan (Villa Fc), Abdulhakim Khamis Faki (Sporting FC), Abubakar Suleiman (ZFDC), Mudathir Nassor (New Afrika), Salum Suleiman (Kimbunga Fc) Ahmada Khamis Amour (Kinyasini), Shaabani Pandu (Villa United), Omar Haji Chareli (Mlandege), Abdul salami Habibu Ubwa (Villa United) na Ame Ali Khamis (Villa United).

Viungo: Yussuf Nassor “Bwanga” (ZFDC), Imrani Mohd Abdallah (Muembe beni), Hassan Hamid (Mwambao), Arif Mohd Said (Opec), Fahad Mussa Hassan (Mapembeani), Eliyass Suleiman (KMKM), Nassir Sheha Abdallah (Opec), Mohd Mussa (Malindi), Yahaya Silima (ZFDC), Abdul hakim Naimu (Villa United), Khalid Habib Iddi (Mpapa Star), Mohd Ramadhan Khamis (Villa United), Mohd Issa Simai (Happy kids), Bakar Ajuwed Jaffar (JKU Academy) na Rakib Mohd Ali (Freedom Kids).

Washambuliaji: Faki Abdallah (JKU Academy), Hussein Mohd Khamis, (New Afrika), Said Salum Khamis (Taifa ya Jangombe), Mohd Daud Suleiman (King Boys), Abdillah Haji Khamis (Opec), Ibrahim Ali “Chafu” (Mlandege), Omar Ame Omar (Kwerekwe City), Abdul hamid Juma “Samata” (Mlandege) na Ramadhan Makame (Yambone).

Wachezaji hao watafanyiwa mchujo na kubakisha wachezaji 25 kuunda timu ya Taifa ya U20 ya Zanzibar.

Aidha kocha Salum Ali amesema wachezaji hao waje na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa  wawe wamezaliwa January mwaka 2000 ili kupata umri sahihi.

Kwa upande mwengine amesema watahakikisha watazingatia umri sahihi wa mchezaji nidhamu ya mchezaji na na uwezo wa mchezaji kwa kiwango chake.