Rais msataafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Marisho Kikwete ametoa pole kwa familia na wanachana wa CUF kufuatia kifo cha katibu mkuu wa chama hichi Khalifa Suleiman na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hichi kigumu.

Rais Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema “Ni kweli tulikuwa pande mbili tofauti lakini kama wanadamu tulikuwa marafiki tangu wakati tukiwa wote Bungeni na hata baada ya Mimi kuacha Ubunge. Daima nitamkumbuka kwa moyo wake wa upendo, ukarimu, ucheshi na huruma. Tuko pamoja katika majonzi na kuomboleza”