Maafisa wa Polis nchini Ethiopia wamekamata kilo 3,300 za bangi- ikiwa ni mojawapo ya shehena kubwa zaidi ya bangi kuwahi kunaswa na maafisa hao wa usalama wa nchi hiyo.

Kwa mujibu ya ripoti iliyotolewa na shirika la utangazaji la FBC, shehena hiyo ya bangi ilinaswa mapema siku ya jana viungani mwa mji wa Addis Ababa ikiwa inasafirishwa na mojawapo ya magari ya mizigo.

Hata hivyo si mara ya kwanza kwa shehena kubwa ya bangi kukamatwa nchini humo, inaelezwa kuwa mnamo Aprili mwaka huu, maafisa wa usalama wa Ethiopia waliripoti kukama kilo 48 ya dawa ya kulevya aina ya cocaine.