Katiaka nchi ya Msumbiji watu zaidi ya 15,000 wanahitaji kuokolewa haraka na kupewa hifadhi kutoka na kimbuga kilichopewa jina la Idai, kilichosababisha vifo vya mamia ya watu.

Inaarifiwa kuwa watu wengi wamekwama juu ya mapaa ya majengo, na juu ya miti baada ya kupoteza makaazi yao.

Watoa misaada wanasema kuwa mji wa Beira ambao umeharibiwa na kimbuga hicho, kilichosababisha upepo mkali na mafuta, huenda ukawa salama kwa siku mbili au tatu zijazo baada ya maji kuondolewa.

Hadi sasa idadi ya watu walipoteza maisha nchini Msumbiji ni 300,lakini inahofiwa kuwa huenda idadi ikaongeka. Kimbunga hiki kimesababisha madhara makubwa katika nchi jirani ya Zimbabwe na Malawi ambako vifo vya watu vimeripotiwa.