Mwalimu mkuu wa skuli ya Kinuni Sekondari anadaiwa kutaka kufanya kitendo cha udhalilishaji cha kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 17 jina linahifadhiwa ambaye alikuwa mwanafunzi wake.

Tukio hilo limetokea nyuma ya skuli ya msingi Magogoni wilaya ya Magharibi B Unguja majira ya saa 4 usiku, Mwalimu huyo alikutwa katika harakati za kutaka kufanya kitendo hicho ndipo wapita njia walisikia kishindo na waliposogea eneo la tukio ambapo baada ya mvutano na wananchi mwalimu huyo alikimbia na kuingia vichakani.

Akizungumzia tukio hilo Sheha wa Shehiya ya Magogoni Abdulwahid Mohammed Ahmada amesema mtuhumiwa anajulikana kuwa ni mwalimu mkuu wa skuli ya Kinuni wilaya ya Magharib B Unguja kwani kabla ya kikimbia eneo la tukio mwalimu huyo alipigwa picha na aliaacha vespa yake eneo la tukio.

Nae mkuu wa wilaya ya Magharibi B Kepteni Silima Haji wa Haji amesema kesi imesharipotiwa polisi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo “Kama Mwalimu anafika kufanya kitendo kama hichi cha kumdhalilisha mtu mwengine pengine kwasababu alikuwa mwanafunzi pale, hatakama sasa hasomi tena inamaana hili jambo ilikuwa ni mazoea yake” Amesema  Kepteni Silima.

Hadi inaripotiwa taarifa hii Mtuhumiwa huyo yupo chini ya ulinzi wa Polisi.