Kufuatia kupotea kwa kiongozi wa klabu ya Simba na mmiliki wa kampuni ya Metl Mohamed Dewij alimaarufu Mo Dewij klabu ya Simba imeamua kuahirisha mazoezi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Afisa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara,amesema “Uongozi wa klabu ya Simba kwa mashauriano na Benchi la Ufundi la klabu yetu,chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems limeamua kuhairisha mazoezi ya Timu leo,ili kutoa fursa kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kushiriki ipasavyo kwenye Dua na Sala kwa ajili ya kiongozi wetu MO”

 

Hadi asubuhi hii ya leo hakuna taarifa zozote zilizotolewa za kupatikana kwa kiongozi huyo mkubwa wa klabu ya Simba pamoja na mmiliki wa kampuni ya METL ambayo inafanya biashara zake katika baadhi ya nchi barani Afrika.