MABAHARIA wa KMKM wanaendelea kujiweka katika nafasi ngumu ya kutwaa ubingwa wa Zanzibar, baada ya juzi kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Malindi.

Mchezo huo wa ligi kuu Zanzibar ulipigwa katika dimba la Amaan, kipigo ambacho kinaweza kuipoteza dira timu hiyo katika harakati za kuwania ubingwa wa Zanzibar.

KMKM iliongoza ligi kwa muda mrefu lakini ktikaa mechi za hivi karibuni imeonekna ikipoteza muelekeo kwa kupoteza baadhi ya michezo.

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Amaan majira ya saa10:00 jioni ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu hizo.

Bao pekee la Mlaindi lilifungwa na kwa kichwa na Ibrahim Abdalla dakika ya 24, ambalo lilidumu hadi dakika 90 za mchezo huo.

Kurudi tena katika kipindi cha pili cha lala salama timu hizo ziliingia na mabdiliko makubwa kwa kila mmoja kuta kuzifumua nyavu za mwenzake,lakini hadi mchezo huo unamalizika hakuna timu iliongiza bao kwa mwenzake.

Mchezo mwengine uliopigwa uwanja wa Moa Zedong kati ya Polisi Chuoni, hadi mchezo unamalizika Polisi iliichapa Chuoni mabao 2-1.